Tuesday, April 25, 2017

VIUMBE WAKOSEKANA KATIKA ANGA ZA JUU


Kiumbe wa anga za juu

Wataalamu wa masuala ya sayansi wanaotafuta maisha katika anga za juu watahitajika kusubiri zaidi

Mradi huo wa gharama ya dola milioni 100 wa kutafuta dalili za viumbe wa anga za juu bado haujapata chochote mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa.

Shughuli hiyo inafanywa kwa kutumia darubini kubwa ambayo inasikiza dalili yoyote ya kuwepo viumbe vya angani.

Wanasayansi walitoa visa 11 ambavyo vilitarajiwa kuonyesha dalili za maisha angani lakini tena wakaamua kuwa vilitoka kwa binadamu.

Prof Stephen Hawking anasema kuwa huenda kuna maisha katika anga za juu

Mradi huo ni wa miaka kumi unaoungwa mkono na watu kama Prof Stephen Hawking.

Darubini hizo zina uwezo wa kutafuta dalili za kuwepo teknolojia ambayo iliundwa na viumbe vilivyo nje ya sayari ya dunia.

Darubini hii iliyo West Virginia, Marekani ni moja ya darubini zenye nguvu zaidi duniani

Mwaka uliopita mradi huo ulifuatilia nyota kwa jina Tabby ambayo ilikuwa na tabia iliyosababisha watu wafakiri kuwa ikuwa na maisha.

Hata hivyo iligundulwia kwa hali hiyo ilisababishwa na nyota wengine walichangia nyota hiyo kuwa na halili kama hizo.

No comments:

Post a Comment