Wednesday, April 5, 2017

SURA MPYA YA RAIS JOSEPH KABILA

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila amesema kuwa atamteua waziri mkuu ndani ya saa 48 zinazokuja wakati akihutubia wabunge mjini Kinshasa.

Hata hivyo Rais Kabila leo ameoneka akiwa na sura tofauti kinyume na kawaida yake. Kabila ambaye kawaida hunyoa nyele kabisa, leo ameoneka akiwa na nywele nyingi kichwani pamoja na masharubu.

Wadhifa huo wa waziri mkuu utashikiliwa na mwanachama upinzani kama sehemu ya makubaliano yaliyoongazwa na kanisa katoliki.

Kabila pia aliahidi kuandaa uchaguzi baadaye mwaka huu lakini hakutangaza tarehe kamili.

No comments:

Post a Comment