Simba ikicheza kwenye Uwanja wa Kaitaba, ilikubali kipigo cha mabao 2-1
na kujikuta ikiteremka mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Akizungumza na mashabiki wa Simba katika tawi la timu hiyo mkoani hapa,
Meneja wa klabu hiyo, Mussa Hassan 'Mgosi' alisema hakuna haja ya
kutafuta mchawi na kuwataka mashabiki kusahau matokeo hayo na kuangalia
michezo ya mbele.
"Ni matokeo ya kuumiza lakini ndio mpira, tunawaomba radhi mashabiki wote ambao wameumizwa na matokeo yetu," alisema Mgosi.
Aidha, Mgosi aliwatoa hofu mahabiki wa timu hiyo na kusema Simba
imejipanga kushinda mechi mbili zilizobakia mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mgosi alisema kikosi cha timu hiyo kitapumzika kwa siku tatu mkoani hapa
kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa dhidi
ya Mbao FC utakaochezwa Aprili 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCm
Kirumba.
No comments:
Post a Comment