Wednesday, April 5, 2017

BASI LA TFF LILILOTUMIWA NA SERENGETI BOYS LAACHIWA


Mamlaka ya mapato nchini, TRA imeliachia basi la shirikisho la soka nchini, TFF lililokuwa limekamatwa na wakala wake wa udalali, Yono kutokana na limbikizo la madeni. Kampuni ya Yono ililishikilia kwa muda basi hilo jana.

Taarifa ya TFF kupitia mitandao ya kijamii imesema: Nathibitisha kuwa Kampuni ya Udalali ya Yono ambayo ni Wakala wa TRA imetangaza kuliachia gari mara moja basi linalotumiwa na wachezaji wa Serengeti Boys na wameomba nilifuate hata sasa, usiku huu. Wamefuata amri ya TRA. Tutalifuata asubuhi, ili liendelee na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka vijana wetu Airport kuwahi ndege kwani vijana wetu wanatarajia kuondoka jioni.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametweet: Basi la TFF limeachiwa usiku huu.Suala hili la kodi tukijaliwa tutalimaliza vizuri tu kwa majadiliano.Usikimbilie kuhukumu.”

Awali wao wenye TRA waliandika: TRA inasikitishwa na kitendo cha mmoja wa mawakala wa kudai madeni kwa kukamata gari ya Serengeti Boys bila kujali wala kuzingatia utaratibu. Imethibitisha agizo la kuachiwa kwa gari hiyo limetekelezwa, wakati taratibu zingine za kiutendaji zikiwa zinaendelea kwa wahusika.

No comments:

Post a Comment