KENYA:MTU MMOJA AMEUWAWA BAADA YA KURKA UZIO NA KUINGIA KWENYE IKULU YA KENYA
Walinzi wa Rais walimpiga risasi na kumuua mtu aliyeingia kwenye ikulu
ya Kenya, Jumapili ya majuzi wakati Rais Uhuru Kenyatta akihudhuria
mashindano ya golf huko Muthaiga, kwa mujibu wa gazeti la Sunday Nation.
Katika tukio hilo ambalo limebaki kuwa siri kubwa wakati uchunguzi
ukiendelea, mtu huyo asiyefahamika na mwenye umri wa makamo, alidaiwa
kuingia bila ruhusa kwenye maeneo yanayolindwa vikali kabla ya saa 11
jioni na alikuwa kwenye eneo la maegesho, si mbali sana na jengo lenyewe
na ndipo walinzi walipomuona.
Vyanzo vimeliambia gazeti hilo kuwa maafisa wa usalama wanaamini mtu
huyo aliruka uzio wa ikulu hiyo sababu haiwezekani kuingia ndani bila
kupita getini ambako nako hadi uruhusiwe.
Hii ni mara ya kwanza mtu yeyote kupigwa risasi na kuuawa ndani ya
viwanja vya ikulu, lakini hilo ni tukio la tatu kwa mtu kuingia bila
ruhusa tangu Rais Kenyatta ahamie humo mwaka 2013.
Chanzo kimoja kimesema mtu huyo alikuwa na kisu na kingine kudai hakuwa
na silaha. Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
jijini Nairobi na hadi Ijumaa hakukuwa na mtu aliyeenda kuulizia.
No comments:
Post a Comment