Thursday, April 27, 2017

BURUNDI YAKATAA MSAADA KUTOKA RWANDA


Serikali ya Burundi imesema, imezuia uingizwaji wa chakula cha msaada kutoka Rwanda kwa sababu za kiusalama

Msemaji wa jeshi la polisi la Burundi Pierre Nkurinkiye ameikumbusha jumuiya ya kimataifa madai ya serikali ya Burundi dhidi ya Rwanda kutokana na nchi hiyo kuhusika katika uvunjifu wa amani nchini Burundi.

Bw. Nkurikiye amesisitiza kwamba, watu na vitu mbalimbali vilivyotoka Rwanda vimetumika kuvuruga usalama wa Burundi tangu mwaka wa 2015,

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Burundi na Rwanda umepelekea nchi ya Burundi kupiga marufuku misaada ya vyakula vilivyonunuliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP)  katika maghala ya Rwanda.

Msafara wa malori ya shirika hilo yameamrishwa kurudi nchini Rwanda Jumanne baada ya kuzuiliwa kwenye mpaka baina ya nchi hizo kwa siku kadhaa.

No comments:

Post a Comment