BEKI WA SIMBA, ABDI BANDA.
Uamuzi wa Banda kurejea uwanjani umetolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo imetangaza kumfungia beki huyo mechi mbili kutokana na kosa lake la kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla katika mechi iliyowakutanisha iliyofanyika Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Taarifa kutoka kwenye kikao hicho ambacho Banda aliitwa kuhojiwa kilieleza kuwa adhabu ya beki huyo ni kutocheza mechi mbili.
Awali beki huyo wa Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) alisimamishwa kwa muda usiojulikana na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania maarufu Kamati ya Saa 72.
Hatua hiyo ilimfanya beki huyo ashindwe kuitumikia timu yake katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara zilizopita ambazo Simba iliikabili Mbao FC na kupata ushindi wa mabao 3-2 na dhidi ya Toto Africans ambayo walitoka sare ya bila kufungana. Mechi zote zilifanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kama pia ilibaini Banda ambaye hakupewa adhabu yoyote na refa kwa sababu hakuona tukio hilo, alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi namba 169 kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akimpiga kiungo Said Juma ‘Makapu’.
Awali, Klabu ya Kagera Sugar iliwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo
cha beki wa Simba, Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla
wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua
yoyote.
No comments:
Post a Comment