Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza
wakuu wote wa vyuo nchini kuwatambua wanafunzi wao wanaojihusisha na
matumizi ya dawa za kulevya na kupeleka taarifa kwake.
Profesa
Joyce Ndalichako ambaye ni mjumbe wa Tume ya Kudhibiti Dawa ya kulevya
kutokana na wadhifa wake ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao
cha kazi cha wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDCs)
kilichofanyika katika ukumbi wa Veta mjini hapa.
Amesema
agizo hilo amelitoa kwa wakuu wa vyuo vyote nchini kuona kuwa wanakuwa
makini kuhakikisha kuwa kwanza vyuo vyao havigeuzwi kuwa vijiwe vya watu
wanaotumia madawa ya kulevya lakini pili kuwatambua vijana wote
wanaosoma katika vyuo vyao kama wanatumia madawa ya kulevya.
“Kama
serikali tumejiwekea malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025 kwa kujenga viwanda na rasilimali kubwa tunayoitegemea ni vijana
wetu walioko mashuleni, hivyo kama juhudi za makusudi hazitafanyika
katika kupambana na madawa ya kulevya malengo yetu hayatafikiwa kwa kuwa
madawa ya kulevya yanaharibu vijana wetu,” alisema Profesa Ndalichako.
Amesema
vijana wengi walioko vyuo vikuu wameharibikiwa kutokana na madawa ya
kulevya hivyo nguvu kubwa inahitajika katika mapambano hayo ili
kulinusuru taifa kwa kuwa wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kubwa ya
kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inafikiwa.
“Hii
vita ya madawa ya kulevya siyo ya lelemama inatakiwa ujitoe mhanga kwa
kuwa tunapambana na watu wenye nguvu,” alisema Profesa Ndalichako.
Mbali
na hilo ameviagiza vyuo vya maendeleo ya Wananchi kuhakikisha kuwa
vinajitangaza kwa jamii ili vionekane kuwa vipo kwa kuwa vyuo vingi
havina wanafunzi wa kutosha huku ikibainika kuwa chuo kimojawapo
(hakukitaja jina) kina mwanafunzi mmoja tu.
No comments:
Post a Comment