Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amemtaka
Mkurugenzi wa Habari maelezo kufuatilia utendaji kazi wa maafisa habari
na mawasiano wote ili kuona utendaji kazi wao kama unaleta maendeleo kwa
jamii.
Waziri
huyo ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na maafisa habari na
mawasiliano wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano
wa Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo Mkoani Dodoma.
Amesema
kuwa wao ndiyo chanzo cha kuwafanya viongozi wao kukimbia vyombo vya
habari kutokana na maafisa hao kushindwa kuwaandaa vyema badala ya kutoa
habari zinazotakiwa kwa jamii.
Amesema
kuwa maafisa habari na viongozi wa umma nchini wanapaswa kutekeleza
sheria hasa zinazowataka kutoa habari na taarifa kwa kuhakikisha vyombo
vya habari na wananchi wanapata habari kwa wakati bila urasimu.
“Nataka
niiagize ofisi ya mkurugenzi wa habari maelezo kuhakikisha kuwa
mnafuatilia utendaji kazi wa kila afisa habari na mawasiliano ili
kujiridhisha kama wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria au la na kama
tutabaini kuna afisa habari ambaye hatekelezi majukumu yake ipasavyo
tumuombe atupishe”. Alisema Nape
Aidha
Waziri huyo aliwasisitizia maafisa hao kutoa ushirikiano mzuri kwa
waandishi wa habari pindi wanapofika katika ofisi zao kuwapa taarifa
sahihi na kwa wakati ili jamii iweze kupata ufumbuzi ya matatizo yao.
No comments:
Post a Comment