Wednesday, March 15, 2017

WANASHERIA WA MANJI WAWASILISHA MAOMBI APANDISHWE KIZIMBANI KWA KESI YA UHAMIAJI

Wakati Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji anapanda tena Mahakama ya Kisutu kujibu kesi ya tuhuma za madawa ya kulevya, wanasheria wake wamesilisha hati ya maombi kutaka apandishwe kizimbani kwa kesi ya uhamiaji.

Taarifa zinaeleza, wanasheria wa Manji wamewasilisha hati hiyo mahakamani wakitaka apandishwe mahakamani kwa kesi ya uhamiaji ambao wanamtuhumu kuingia nchini kinyume na sheria.

Manji amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini chini ya ulinzi wa Maofisa wa Uhamiaji pamoja Jeshi la Polisi.

Hata hivyo kwa zaidi ya wiki tatu sasa, hajawahi kupandishwa kizimbani. Hali iliyosababisha wanasheria wake kuwasilisha hati hiyo ya maombi.

No comments:

Post a Comment