Siku ya Jumannne majira ya jioni rais wa Marekani Donald Trump alimpigia
mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta na kubadilishana mawazo kuhusu
uhusiano baina ya nchi hizo mbili,biashara,masuala ya kikanda na
mapambano dhidi ya ugaidi.
Uhuru Kenyatta ni rais wa tatu kutoka bara la Afrika aliyepata simu ya rais Trump tangu kuingia madarakani Januari 20 mwaka huu.
Rais Trump alimuhakikishia Uhuru kuwa Marekani itatoa msaada kwa Kenya katika kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab .
Aidha Trump alisema kuwa serikali yake ina mipango ya kuboresha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Viongozi hao wawili pia walijadiliana kuhusu ushirikiano wa kibiashara
na uchumi na jinsi watakavyokabiliana dhidi ya changamoto kuu ya usalama
.
Trump amefanya mazungumzo ya simu na Uhuru wiki moja baada ya Marekani
kukubalia Kenya kutekeleza safari za ndege za moja kwa moja kutoka Kenya
hadi Marekani.
Hapo awali baada ya kuingia White House,Trump alifanya mazungumzo ya
simu na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na rais wa Afrika Kusini Jacob
Zuma ambapo waliongea kuhusu ushirikiano katika sekta ya uchumi na
usalama.
No comments:
Post a Comment