Lakini moja ya sifa za kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar ni
kuwa na passport ambayo imetolewa na ofisi ya uhamiaji ya Zanzibar kwa
na sio passport zilizotengenezwa Tanzania bara.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa ZFA Ali Bakar ‘Cheupe’ amesema kuwa
wachezaji watakaoitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar ni kwa wale ambao
Pasipoti zao zimetengenezwa visiwani Zanzibar.
“Wachezaji ambao wana sifa ya kuichezea Zanzibar Heroes ni wale ambao
Pasipoti zao wamezipata Zanzibar, yani Pasipoti yake imetolewa hapa hapa
Zanzibar,” alisema Cheupe.
Kwa maana hiyo, wachezaji wote wa Zanzibar ambao Passport zao
zimetengenezwa Tanzania bara hawatakuwa na sifa ya kuitumikia Zanzibar
Heroes.
Machi 16, 2017 ilikuwa ni siku nzuri na yenye historia kubwa kwa
Zanzibar baada ya kuingizwa rasmi kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la
Soka Barani Afrika ‘CAF’ kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa
Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia baada ya
kukubaliwa kwa kura 51 kati ya 54 zilizopigwa na nchi wanachama wa CAF.
No comments:
Post a Comment