Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Godfrey Ngupula ameshangazwa na
ujasiri walionao wananchi wanaolima mashamba makubwa ya bangi kwa
kujiamini kama hakuna serikali.
Akizungumza na wanahabari wakati akiwa kwenye operesheni ya kukamata na
kuteketeza bangi,alisema baadhi ya wananchi wamegeuza hifadhi ya Igombe
iliyopo mpakani mwa wilaya za Nzega kugeuzwa kuwa mashamba ya bangi.
“Sijawahi kuona watu wanalima bangi kwa kujiamini kiasi hiki tena kwa wingi kama hakuna Serikali, tutahakikisha bangi yote inateketezwa na watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani,” alisema Ngupula
Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nzega, Costantine Mbogambi alisema jeshi hilo litapiga kambi msituni kuhakikisha mashamba yote yanateketezwa.

No comments:
Post a Comment