SIMBA YATAMBA KUOKOA NYASI ZAKE TRA
Hatimaye Klabu ya Simba SC yajitokeza hadharani na kukiri kudaiwa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kodi za nyasi bandia walizozitelekeza
bandarini huku wakifurahia kuongezewa muda wa kulipa malipo hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni ya udalali ya MAJEMBE AUCTION
kutangaza kuzipiga mnada endapo klabu hiyo itashindwa kwenda kulipia
ushuru unaodaiwa.
"Simba inakiri kudaiwa na TRA kodi ya nyasi bandia, tunafanya juhudi
zote kulipa kodi kwa wakati baada ya kuomba kuongezewa muda kulipa na
TRA". Imeandika klabu hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ya twiiter
pamoja na instagram asubuhi ya leo (Ijumaa).
Pamoja na hayo klabu hiyo imewataka mashabiki na wanachama wake
kuendelea kuwapa ushirikiano katika mechi zao za kanda ya ziwa vile vile
kupuuza maneno ya mitandaoni yanayoweza kuwa na lengo baya kwa Simba
SC.
Huu ndiyo ujumbe wao
No comments:
Post a Comment