Mchezo umepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Huo utakuwa mchezo wa pili kwa timu hizo kukutana katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya Septemba mwaka jana kucheza kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa na Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Akizungumza na gazeti hili jana Mjini hapa, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (Dorefa) Hamis Kissoy, alisema wameamua kuileta Simba mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhamasisha soka mkoani humo pamoja na kukata kiu ya mashabiki wa soka mkoani humo kutaka kuiona timu hiyo.
‘’Tumeanza na Simba, tupo mbioni kuwaleta Yanga ili kukata kiu ya mashabiki wa Dodoma ambao wanataka kuwaona baadhi ya wachezaji, kwa Simba huu utakuwa mchezo wa maandalizi kwao kuelekea kwenye michezo ya mbele yao ya Ligi Kuu," alisema Kissoy.
Kwa upande wake Kocha wa timu ya Polisi Dodoma, Paul Pweza, wanajiandaa kwa ajili ya mchezo huo ambao kwao utakuwa kipimo kizuri kwa wachezaji wao.
‘’Tunakikosi madhubuti, tutaangalia baadhi ya wachezaji tutakaowatumia katika Ligi daraja la kwanza msimu ujao na huu mchezo utakuwa sehemu ya kipimo kwao’’alisema Pweza.
No comments:
Post a Comment