NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta
ameondoka kurejea Ubelgiji na hatakuwepo kwenye kikosi kitakachomenyana
na Burundi leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samatta aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana
Jumamosi, amelazimika kurejea ili kuwahi maandalizi ya klabu yake kwa
mchezo wa Robo Fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Celta de Vigo
nchini Hispania Aprili 13.
Kwa kumkosa Samatta, kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuanzisha
Ibrahim Hajib kama mshambuliaji kiongozi akicheza na kiungo Farid Mussa,
huku pembeni akiwatumia kiungo Muzamil Yassin kulia na winga Simon
Msuva kushoto.
Kwa ujumla kikosi cha Stars leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary
Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid
Mao, Muzamil Yassin, Salum Abubakr ‘Sure Boy’, Ibrahim Hajib, Farid
Mussa na Simon Msuva.
Katika benchi watakuwapo Said Mohammed, Hassan Kessy, Gareiel Michael,
Hassan Kabunda, Jonas Mkude, Mbarak Yussuf, Abdulrahman Juma, Shiza
Kichuya na Frank Domayo.
1. Deo Munishi
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Abdi Banda
5. Salim mbonde
6. Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. Farid Mussa
10. Abubakary Salum
11. Ibrahim Ajib
No comments:
Post a Comment