WINGA wa timu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini
Hispania, Farid Musa amesema anashukuru sana sapoti anayopewa na nahodha
wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye amekuwa akimtaka kuwa mvumilivu
katika maisha ya soka la kimataifa la sivyo hatofika kokote.
Farid ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Stars waliocheza mchezo
wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana juzi Jumamosi, licha ya
kutokea benchi alionesha kiwango cha juu kwa dakika chache alizocheza
kipindi cha pili.
Shaffihdauda.co.tz ilipiga story na Faridi Musa ambaye alisema “Mara
kadhaa Samatta nimekuwa nikiwasiliana naye na kunisisitiza kuendelea
kuwa mvumilivu kwakuwa hakuna kitu kinachopatikana bila kukitolea jasho
kwa wakati huu unapowaza kufanikiwa kama Cristiano Ronaldo ama Lione
Messi.”
“Samata amenisihi sana niwe mvumilivu kwani anajua ugumu wa soka la
Ulaya, lina mambo mengi na ili ufanikiwe jitihada na uvumilivu wa hali
ya juu unahitajika,” alisema Farid.
Farid ambaye bado hajaanza kucheza kikosi cha kwanza katika klabu hiyo
kutokana na kutokuwa na utimamu wa mwili akiwa kwenye kikosi cha pili
alisema anakubaliana moja kwa moja na Samatta kuwa uvumilivu unahitajika
ili kufanikiwa.
No comments:
Post a Comment