Kiungo
mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, ameweka wazi kuwa bao
alilofunga kiungo wa Simba, Ibrahim Ajibu siyo la halali kutokana na
mazingira ya lilivyopatikana ambapo anaamini haikuwa faulo kama maamuzi
ya mwamuzi yalivyokuwa.
Ngassa
alikuwa sehemu ya kikosi cha Mbeya City ambacho kilitoka sare ya mabao
2-2 na Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ambao ulipigwa Uwanja wa Taifa,
Dar. Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Ditram Nchimbi na Kenny Ally
wakati yale ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajibu na Shiza Kichuya kwa
penalti.
Ngassa
ambaye amewahi kuzichezea Yanga, Azam na Simba kwa nyakati tofauti,
amesema kwamba bao hilo la Ajibu halikuwa halali kwa sababu hakukuwa na
faulo yoyote ambayo ilifanywa na mabeki wa timu hiyo kwa kiungo Mohammed
Ibrahim ‘Cabaye’.
“Lile
bao la Ajibu siyo halali kwa sababu hatukufanya faulo yoyote kama
mwamuzi alivyodai kwa sababu beki wetu alizuia mpira na siyo kumchezea
rafu Mohammed Ibrahim ambaye alianguka na mwamuzi akaruhusu kupigwa
faulo hiyo ambayo iliipa Simba bao.
“Lakini
bao la pili ambalo walilipata kwa penalti wala sina shaka nalo kwa
sababu mchezaji wao alifanyiwa faulo kweli kwenye eneo la hatari ambalo
lazima pigo hilo litolewe.
“Lakini
kiukweli mechi ilikuwa nzuri na kila timu ilikuwa na nafasi ya kushinda
lakini mwisho ndiyo matokeo hayo yametokea lakini tunaenda kujipanga
kwa ajili ya mechi zinazokuja ambazo naamini tutafanya vizuri,” alisema
Ngassa ambaye ametokea Fanja ya Oman kabla ya kutua Mbeya City.
No comments:
Post a Comment