Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri mpya ya kupiga marufuku
wahamiaji kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani, katika amri
iliyotolewa awali na kuzuiwa na mahakama ilizitaja nchi saba, lakini
sasa Iraq imeondolewa kwenye orodha ya sasa.
Serikali ya Marekani inasema nchi zilizoorodheshwa zinafadhili ugaidi au
zimeshindwa kupambana na magaidi wanayofanya shughuli zao ndani ya nchi
zao.
Wakosoaji wa mpango huu wa Trump wamesema kuwa hatua hii inakwenda
kinyume na Katiba kwa kuwa msingi wake umeegemea kwenye ubaguzi wa
kidini.
Nihad Awad kutoka Baraza la Kiislam nchini Marekani linalotafuta kujenga
mtazamo chanya wa dini ya kiislamu nchini humo, amesema watapambana
dhidi ya Amri hiyo
Naye Kaimu mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za wamarekani "
American Civil Liberties Union "Lee Gelernt amesisitiza kuwa amri hii
haiiweki Marekani mahala salama
''hatufikiri kuwa amri hii ni muhimu kwa usalama wa taifa,lakini si sisi
tunaosema hivyo , ni wataalam wa masuala ya usalama na wanadiplomasia
wanaoheshimika kutoka uongozi wa Democratic na Republican ambao awali
walichukua hatua za kufungua shauri mahakamani wakipinga amri hii
wakisema haita tufanya kuwa salama, zaidi ya yote tunaona nakala
iliyovuja kutoka idara ya mambo ya ndani, maafisa wakisema kuwa mpango
huu hautasaidia usalama wa taifa letu''
Nchi zilizoorodheshwa kwenye amri hii mpya ya Donald Trump ni Iran,
Sudan, Syria, Libya, Somalia na Yemen.Mwanasheria mkuu wa Serikali Jeff
Sessions, ameviambia vyombo vya habari kuwa nchi tatu kati ya
zilizotajwa zinafadhili ugaidi na nyingine tatu zimeshindwa kabisa
kupambana na wanamgambo kama vile Islamic State na Al Qaeda.
No comments:
Post a Comment