CHADEMA tunasema hivi, Rais Magufuli acha mchezo wa kucheza na maisha ya
madaktari wetu, katika mazingira ya kawaida, ingekuwa wanakwenda Kenya
wakati kuna hali ya utulivu, kuna hali ya uhakika wa Usalama Kenya
tungeruhusu vijana wetu wakafanye kazi kwa sababu hata Wakenya ni ndugu
zetu, lakini katika mazingira ambayo kuna mgomo Kenya, kuna kutoelewana
kati ya Serikali ya Kenya na madaktari wao, sisi ndio tuwe kimbelembele
cha kuwatoa watoto wetu kwenda kutibu Kenya wakati Wakenya wenyewe
hawawataki ni kuweka maisha ya Watanzania wenzetu , wataalam wetu katika
risk, sisi Kama Chama Kikuu cha Upinzani tunapinga, na naomba Mkutano
huu Mkuu wa Kanda ya Pwani utoe tamko la kupinga madaktari wetu kwenda
nchini Kenya.
Magufuli na Serikali yake wawape ajira vijana wetu vituo vya afya havina
madaktari, Sera yetu ya Taifa inasema vituo vyetu vya afya lazima
vihudumiwe na madaktari lakini mpaka leo hakuna madaktari kwenye vituo
vya afya kwa sababu Serikali imeshindwa kuajiri.
Kwa hiyo wapo vijana wengi kwa muda wa miaka miwili hawajaajiriwa lakini
suluhu sio kuwakimbizia nchi za jirani ambazo zina migogoro na wataalam
wao, suluhu ni Serikali yetu itafute fedha iwaajiri vijana hawa, mama
zetu, wazee wetu, vijana wetu wanawahaitaji madaktari hawa wawatibu
katika vituo vyetu vya afya katika zahanati zetu katika hospitali zetu,
Kwa hiyo naomba Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda Pwani, naomba mnikubalie
Kama Mwenyekiti wa Chama kupitia Mkutano huu tutoe tamko hili rasmi la
kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment