SARAKASI na vuta nikuvute za uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS) litafikia tamati leo baada ya wanachama kutoa ‘hukumu’ juu ya
nani watashika hatamu za uongozi.
Wakati uchaguzi huo ukifanyika leo, jana ulizuka mjadala mkali wakati wa mkutano huku baadhi ya wanachama wakitaka Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, afutwe uanachama.
Tangu kutangazwa kufanyika uchaguzi huo na kujitokeza watu mashuhuri katika tasnia hiyo na siasa wakiwamo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha kupitishwa kugombea urais, kumekuwa na vuta nikuvute hata serikali kutishia kukifuta chama hicho kwa kile ilichodai kuingiliwa kisiasa.
Hata hivyo,habari zilizotufikia wakati tukienda mitamboni,zilieleza kuwa Masha ametangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Lissu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, alitoa tishio hilo ambalo lilizua hali ya kutoelewana baina ya serikali na wanachama wa TLS huku wakimtaka waziri huyo ajiuzulu kwa kauli yake hiyo.
Mbali na kauli ya Dk. Mwakyembe kutishia kuifuta TLS, baadhi ya wanachama walifungua kesi mahakamani Dar es Salaam na Dodoma wakitaka uchaguzi huo usimamishwe kwa madai ya kukiukwa kwa katiba ya chama. Hata hivyo kesi hizo zilifutwa na hatimaye mkutano mkuu wa TLS ukaanza jana.
Kwa mantiki hiyo, kufanyika kwa uchaguzi huo leo kutahitimisha migongano, malumbano na vijembe vilivyokuwa vimetawala miongoni mwa wadau wa tasnia ya sheria Tanzania.
Katika mkutano huo jana, mjadala mkali uliibuka kwa baadhi kutaka Dk. Mwakyembe, afutwe uanachama huku baadhi ya wanasheria wakongwe wakimtetea. Mwakyembe ambaye kitaaluma ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, hakuwapo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe waliotaka Dk Mwakyembe afutwe uanachama, walidai ametishia kukifutia usajili chama hicho lakini waliokuwa wakimtetea, walijenga hoja kwamba suala la msingi si yeye isipokuwa wanatakiwa kupigania chama kisifutiwe usajili.
Katika mchango wake, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, alipendekeza mkutano huo ufikie azimio la kumfuta uanachama Dk. Mwakyembe.
“Tumfukuze Mwakyembe TLS, haiwezekeni atoe pendekezo la kukifutia usajili wakati mwenyewe ni mwanachama. Hii inamaanisha nini?” alihoji huku akipigiwa kofi na idadi kubwa ya wanachama walioshiriki mkutano huo mkuu wa mwaka.
Profesa Josephat Kanywanyi, alisema Dk Mwakyembe ambaye ni mwanachama wa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri na mwanachama wa TLS, amejikuta katika wakati mgumu kutoa tishio kama hilo.
Alisema inawezekana tishio hilo likawa limetoka upande wa serikali na yeye Mwakyembe ndiye waziri alipaswa kulitamka, hivyo kuwataka wanachama kujenga hoja za kutetea chama kisifutiwe usajili badala ya kumshambulia mtu.
“Ni jukumu la chama kuhakikisha majukumu yake yanatekelezwa na kuyatetea,” alisema.
Naye Dk. Eve Hawa Sinare, aliwataka wanachama wenzake kutambua kuwa suala la Dk. Mwakyembe si la msingi kwa sasa isipokuwa kupigania chama hicho kisifutiwe usajili.
“Hebu tupiganie chama kisifutiwe usajili, tishio hili linaweza kuwa ni uamuzi wa Baraza la Mawaziri, hakuna anayejua hilo,” alisema.
Dk. Rugeremeleza Nshalla, kwa upande wake alisihi kuepuka kufanya mapambano na badala yake waunde kamati itakayofanya mchakato wa kuifanyia marekebisho makubwa TLS.
Naye Jaji Thomas Mihayo, alisema ingawa kuna tishio la kukifutia usajili TLS, lakini hoja ya kumfuta uanachama Dk. Mwakyembe si sahihi.
“Tuwe makini sana nini cha kufanya. Uamuzi wetu mkubwa ni lazima ufanywe kwa ukomavu. Tuepuke uamuzi wa kufuata mkumbo. Uamuzi wowote tutakaoutoa lazima uonyesha vitu viwili, moja siyo wa uoga bali umetolewa kwa kuzingatia weledi wa taaluma wetu,” alisema na kuwasihi kuepuka mihemko.
Alisema uamuzi wowote utakaochukuliwa kwa mihemko utakuwa na athari kubwa kwao na kwa wanachama wa baadaye.
“Wakati tukisimamia misingi ya utawala wa sheria katika matendo yetu, lazima tujue nani tunayekabiliana naye. Tufanye uamuzi kama wanataaluma wa sheria,” alisema.
Hoja hiyo ya Dk. Sinare iliungwa mkono na Dk. Erick Ng’maryo, na kusisitiza kukifanyia marekebisho makubwa chama hicho. Alisema hatua wanayopaswa kuchukua ni kufanya mazungumzo na serikali na si kupambana nayo.
“Tunapaswa kuzungumza na serikali na siyo kupambana nayo…huwezi kuamka asubuhi na kuanza kupambana nayo isipokuwa kufanya mazungumzo nayo.
“Kwa mfano, unaweza kuamua kwenda kufungua kesi mahakamani, sasa una uhakika gani kama utashinda na ukishindwa hali yako itakuwaje? “Hivi unaweza kulizuia bunge kutunga sheria,” alisema.
Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, kwa upande wake aliunga mkono wazo la kuunda kamati itakayopewa pamoja na mambo mengine kufanya marekebisho ya chama hicho ili kifanye kazi yake vizuri.
Alisema kamati hiyo itaangalia changamoto zilizotolewa na Dk. Mwakyembe na kuangalia muswada ulioandaliwa kupelekwa bungeni na kuzifanyia kazi.
Mapema kuhusu suala la uchaguzi wa viongozi wa chama hicho, Lyod Monuo alitaka wajumbe waahirishe ili kupata muafaka kwanza.
Alisema hakuna sababu ya wanachama kupambana na serikali hivyo ni vyema wakaunda kamati itakayoshughulikia marekebisho ya TLS.
Hata hivyo, ushauri huo ulipingwa na wanachama hao ambao wengi walisikika wakitoa sauti za kuzomea.
Albert Msando, alisema hakubaliani na wazo la kuahirisha uchaguzi huo kwa kuwa uongozi wa sasa umewachosha.
Mapema Allan Isack, anaripoti kuwa, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, jana alishindwa kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa TLS kutokana na tishio lake la kukifuta chama hicho iwapo kitajiingiza katika masuala ya siasa.
Uchaguzi wa viongozi wa chama hicho unafanyika leo jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa TLS, John Seka, alisema, lengo la mkutano huo ni kuweka na kuhakikisha wanasheria wanafanya kazi zao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kujua muktadha wa chama hicho na kufanikisha lengo la wanasheria.
Alisema tishio la kufutwa kwa chama hicho wamekuwa na majadiliano na Serikali, kwani sababu ya kufutwa kwa chama viongozi wa baraza hilo wanalifanyia kazi.
Kuhusiana na kusitishwa kwa uchaguzi, Seka alisema, suala hilo ni la kisheria hivyo hakuna pingamizi lolote kwani uchaguzi umeitishwa na utafanyika kwa mujibu wa sheria.
“Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na hamasa kubwa kutokana na wagombea wanaoshiriki uchaguzi huo wanafahamika zaidi machoni mwa wanajamii hususani katika shughuli zao za kisheria, ambapo alisema kuwa Chama hicho kina haki ya kuendelea na uchaguzi ili kuweza kihitimisha zoezi hilo.
“Uchaguzi wa mwaka huu una hamasa sababu kupitia sheria mpya, tunaweza kufanya uchaguzi mzuri ambao tutapata viongozi wenye uwezo wa kusimamia msingi ya taaluma hii na huwajibikaji kwa watu," alisema.
Alitoa wito kwa wanataaluma ya sheria kufanya kazi kwa kutumia misingi ya kisheria kwa kusaidiana na Serikali, Bunge na Mahakama katika kutunga sheria ili kuongeza nguvu kwa kuwasaidia wanyonge na kuakikisha demokrasia na haki za binadamu zinafatwa.
Kwa upande wake, Dk. Sinare alisema chama hicho kitahakikisha msingi wa kanuni na sheria kwa mujibu wa katiba ya Tanzania inafuatwa bila kujali cheo na dhamana ya mtu.
"Tuwe na wanasheria wa Serikali wanaoweza kumwambia kiongozi yeyote wa Serikali kuwa sheria haitoi mwongozo unaokwenda kinyume na taaluma hiyo,” alisema na kuongeza, TLS itachagua mtu atakayehakikisha misingi ya kisheria inafuatwa japo kuwa watakuwa na wakati mgumu wa kutekeleza adhima hiyo.
"Mtuhumiwa anakamatwa na mwendesha mashtaka wa Serikali kabla ya upelelezi kukamilika na anawekwa kizuizini kwa kipindi kirefu bila kuwapo kwa hoja ya msingi inayomfanya mtu huyo ashikilwe kisheria tafsiri hiyo inaonyesha kuwa uwajibikaji katika sheria Tanzania hakuna," alisema.

No comments:
Post a Comment