Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini ALAT Bwana Gulam Mukadam.
*****
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini ALAT Bwana Gulam Mukadam
amemsimamisha kazi Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Bw Abraham Shemoboyo
kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi milioni 150 za
ufadhili wa jumuiya hiyo mwaka 2015.
Akiongea
katika ofisi za jumuiya hiyo Jijini Dar es salaam, Gulam ambaye pia ni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga amesema, benki ya NMB ilitoa
kiasi hicho cha pesa kwa jumuiya hiyo kwaajili ya ufadhili wa Tuzo ya
Meya (Mayor Awards) na kwamba Katibu huyo hakuwasilisha kiasi chote na
badala yake aliwasilisha shilingi milioni 60 huku kiasi cha shilingi
milioni 90 kikiwa hakijulikani kilipo.
Mukadam
amesema, uamuzi wa kumsimamisha uliamuliwa na kamati tendaji ya ALAT
Taifa na mkutano mkuu wa ALAT taifa, ambapo iliundwa tume ndogo
kuchunguza upotevu wa kiasi hicho cha pesa na kuamuliwa kuwa apishe
uchunguzi dhidi yake kwa upotevu wa pesa hizo.
Aidha
Mstahiki Mukadam amesema, uchunguzi dhidi yake utafanywa na CAG na
kwamba pesa hizo hazikuwekwa kwenye akaunt ya ALAT na badala yake
zilihifadhiwa kwenye akaunti binafsi ijulikanayo kama 'Vision
Investment'.
No comments:
Post a Comment