Akifunguka
jana kwenye kipindi cha Ngazi Kwa Ngazi kinachorushwa na EATV, Diamond
alisema kuwa ‘Salome’ haina matusi bali imebeba lugha ya mahaba mazito.
“Ukiangalia wimbo wa Salome, hauna matusi, ila una maneno ya kimahaba,” alisema Mond.
“Unapozungumzia
wimbo wa kimahaba, matusi yanatokea pale. Matusi yapo kwenye mahaba.
Unapokuwa unaelezea masuala ya kimahaba utaonekana kama unatukana.
Lakini sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu mahaba yale kuyazungumza
katika lugha ambayo ni ngumu sana mtu kuielewa,” alifafanua.
Kwa
upande wake Ray Van, alisema kuwa pamoja na yote yanayosikika kwenye
wimbo ule, wamejitahidi kutumia tafsida kuyaficha na ndio sababu wimbo
ule unapendwa na watu wa rika zote na unaweza kusikilizwa hata katika
jumuiya ya watu wanaoheshimiana.
Salome
ni wimbo uliochukua mahadhi ya wimbo wa zamani wa Saida Kalori ‘Chambua
Kama Karanga’ na umepata nafasi na mafanikio makubwa katika vituo vya
runinga vya kimataifa na kuweka rekodi ya aina yake kwenye mtando wa
YouTube.
Video ya Salome imeangaliwa zaidi ya mara milioni 13 na laki 7 kwenye YouTube.
No comments:
Post a Comment