Mfanyabiashara
maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa
4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.
Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.
Manji
ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na
waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya
Ijumaa.
Manji amewasili na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi huku akiwa na mawakili wake kadhaa.
No comments:
Post a Comment