Waziri
wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe ameendelea kufunguka jinsi
alivyokwama kudhibiti upitishwaji wa dawa za kulevya katika Uwanja wa
Ndege wa Dar es Salaam wakati alipokuwa Waziri wa Uchukuzi hadi kuzidiwa
kete na Agnes Masogange
Waziri
Mwakyembe akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast amesimulia
kilichotokea wakati alipotaka kumdhibiti binti mmoja aliyedaiwa
kupitisha masanduku matano ya 'materials' za kutengenezea dawa za
kulevya aliyekamatwa nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania.
Amesema
baada ya kufuatilia sakata lile mbali na kuchukua hatua kwa watu
waliomsaidia kupitisha mzigo uwanja wa ndege, aliamua kufanya jitihada
za kumkamata binti huyo ili achukuliwe hatua, lakini muda mfupi baada ya
binti huyo kurejea nchini, yeye alihamishwa wizara, hivyo kukosa nguvu
ya kumshughulikia, hatua iliyofanya binti huyo kumfanyia "nyodo".
Kumbukumbu
zinaonesha kuwa binti ambaye alikamatwa nchini Afrika Kusini wakati huo
kwa madai hayo, na kisha Waziri Mwakyembe kumfuatilia hadi kutimua
baadhi ya watumishi wa uwanja huo Mwezi Agost mwaka 2013 alikuwa ni
'video queen' maarufu nchini, Agnes Gerald 'Masogange'.
Vilevile
Mwakyembe amesema kijana wake mmoja anayefahamika kwa jina la Jingu
ambaye yuko gerezani, anapaswa kuongezewa ulinzi kwa kuwa yeye ndiye
aliyekuwa jemedari wa kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, lakini
baadaye aliundiwa kesi na sasa huko gerezani anakutana na watu ambao
wanaweza kumdhuru kutokana na kwamba yeye ndiye aliyesababisha wafungwe.
No comments:
Post a Comment