Thursday, February 23, 2017

UZINDUZI WA TOVUTI 'AFROPREMIERE' YA KUUZA VIDEO ZA MUZIKI WAFAANA






  Wasanii wa muziki wanaendelea kupata namna mpya za kuuza muziki wao. Jumatano hii Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel amezindua tovuti ya afropremiere inayojihusisha na biashara ya kuuza video za wasanii wa muziki mtandaoni.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel (kulia) akiwa na mmoja kati ya wakurugenzi wa tovuti hiyo.

Aidha tovuti hiyo pia imeweka kipengele ambacho kinawanufaisha watayarishaji wa muziki ambao walisahaulika kwa muda mrefu.

Akiongea na wadau pamoja na wasanii waliojitokeza katika uzinduzi huo, Prof.Elisante Ole Gabriel aliwataka wamiliki wa tovuti hiyo kurahisisha mfumo wa malipo wa mtandao huo ili kuepusha usumbufu.

“Kwenye mfumo wa mauzo, muweke mfumo ambao mauzo yakiingia kwenye afropremiere, kuwe na program ambayo itafanya mchanganuo wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki za wasanii, producer na TRA. 

 Hilo litakuwa ni jambo jema na ameniahidi litafanyika,” alisema Prof.Elisante Ole Gabriel.


Prof.Elisante Ole Gabriel akizungumz mbele ya wasanii na wadau waliojitokeza




















No comments:

Post a Comment