Utata
umeibuka juu ya kukamatwa kwa msanii wa filamu nchini Steven Mengele
a.k.a Steve Nyerere, mara baada ya kuwepo kwa taarifa hizo ambazo
zimetolewa ufafanuzi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Simon Sirro.
Akizungumza
jana na wanahabari, Kamishna Sirro alisema yeye hajamuita Steve Nyerere
lakini huenda akawa ameitwa na maafisa wake wa upelelezi kwa ajili ya
mahojiano, jambo ambalo ni sahihi.
Sirro
alisema kuna kikosi maalum alichokipa kazi hiyo na endapo msanii huyo
anahojiwa ataweza kuachiwa kama kikosi hicho kitajiridhisha kuwa
anastahili dhamana, lakini kama kitaona bado kinamuhitaji, kitaendelea
kumshikilia.
Msanii
huyo ameingia kwenye 'headline' hasa mitandaoni baada ya kusambaa kwa
sauti zinazodaiwa kuwa ni mazungumzo kati yake na Mama wa Msanii Wema
Sepetu, kuhusu sakata la dawa za kulevya linalomkabili Wema Sepetu.
Katika
hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alifika katika
kituo hicho kikuu cha polisi Dar es Salaam, na kisha kupandishwa kwenye
gari ya polisi na kupelekwa kusikojulikana.
Kamishna
Sirro alipoulizwa kuhusiana na kinachoendelea kwa mwenyekiti huyo,
alisema kuwa jeshi hilo lina mamlaka ya kumuita Mbowe wakati wowote kwa
ajili ya mahojiano.
No comments:
Post a Comment