RAUNDI
ya Sita ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani
Azam Sports Federation Cup – 2016/17, itaanza Februari 24, 2017 kwa
michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro
mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00 jioni.
Michezo
hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya
Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa kaitaba
mjini Bukoba.
Mechi
nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC
ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali
Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika
saa 1.00 usiku.
Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Jumatano Machi 1, 2017 Simba SC itacheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam wakati Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment