Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjale
ameshusha presha katika kikosi cha timu yake kwani leo Jumamosi
anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi
ya Yanga.
Simba
na Yanga zinatarajiwa kuvaana Jumamosi ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu
Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki
huyo ambaye ameikosa mechi ya Kombe la FA dhidi ya African Lyon,
anaanza mazoezi hayo baada ya kupona majeraha ya enka aliyoyapata kwenye
mechi iliyopita ya ligi kuu dhidi ya Prisons ambapo Simba ilishinda
mabao 3-0.
Akizungumza
jijini Dar, Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema beki huyo ataanza
mazoezi baada ya kupona majeraha hayo yaliyomuweka nje ya uwanja kwa
wiki moja.
Gembe
alisema, beki huyo kabla ya kuanza mazoezi hayo, alikuwa ana program
maalum ya gym huku akiendelea na matibabu hayo ili kuhakikisha anapona
kwa haraka kwa ajili ya kurejea uwanjani.
“Habari
njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa Mwanjale amepona majeraha ya enka
yaliyokuwa yamemuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja sasa.
“Hivyo,
Jumamosi (leo) ataanza mazoezi mepesi binafsi tukiwa kambini Zanzibar
tutakapokwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga.
“Uwezekano
wa kucheza au kutocheza bado haijajulikana kwani ndiyo kwanza atakuwa
anaanza mazoezi, hivyo tusubirie kwanza kwani majeraha aliyoyapata siyo
makubwa sana,” alisema Gembe.
No comments:
Post a Comment