Sunday, February 19, 2017

MANJI SASA ANAKABILIWA NA KESI TATU,NYINGINE YA TIGO YAIBUKA


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ndiye mmiliki mpya wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo.
Manji alinunua kampuni hiyo mwishoni mwa mwaka 2014 na kumalizia malipo mwanzoni mwa mwaka 2015 na kuwa rasmi ya kwake.

Tigo iliuzwa kwenye mnada baada ya wamiliki ambao makao makuu yao ni nchini Sweden kushindwa kumlipa mtumishi wao ambaye alikuwa akiisimamia ambaye ni raia wa Uingereza.

Baada ya Mwingereza huyo kufungua kesi, waajili hao walishindwa kumlipa, hivyo mahakama ikaagiza kufanyika kwa mnada na kampuni nyingine ya nje ikainunua Tigo kabla ya kumuuzia Manji.

Hata hivyo, Manji amekuwa katika misukosuko ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya kutaka mnada urudiwe hali itakayopelekea yeye kupokonywa kampuni hiyo.

“Hii ni kesi ya pili katika zile zinazojulikana ndani ya wiki moja. Lakini wiki iliyopita, kulikuwa na kesi mbili.

“Moja ni ya madawa ya kulevya ambayo wanamtuhumu kuitumia, lakini nyingine ni kuhusiana na kutaka kurudiwa kwa mnada wa Kampuni ya Tigo ambayo ameinunua kwa zaidi ya asilimia 90,” kilieleza chanzo hicho cha uhakika.

“Kama ulikuwa haujui, Tigo ni kampuni ya Manji ambayo aliinunua baada ya Mwingereza aliyekuwa akiisimamia kuwashitaki waajiri wake wa Sweden wamlipe alichokuwa akiwadai. Waliposhindwa, mahakama ikapitisha mnada na kampuni 20 zikajitokeza kununua.

“Kampuni moja ya nje ilifanikiwa kununua na baadaye Manji akanunua hisa kwa asilimia 99. Alilipa kila kitu na hana deni, hivyo tangu mwaka 2014, amekuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano ya Tigo.

 “Lakini kampuni hiyo ya Sweden iliamua kufungua mashtaka Uingereza, ikashindwa. Ikaja hapa imeshindwa na sasa imeamua kukata rufaa tena.

“Hii nilitaka nikueleze tu kuwa Manji amekuwa na kesi tatu ndani ya siku nane zilizopita. Hasa kama kesho atapanda mahakamani ingawa tuna asilimia kubwa atapandishwa na bado hawajatueleza kosa lipi hasa la uhamiaji.”

Hata hivyo, chanzo kilieleza huenda likawa kosa la kuwa na pasi mbili za kusafiria.

“Lile la wafanyakazi, Manji si mmiliki wa kampuni hiyo, labda kama ni lile la pasi mbili analotuhumiwa pia. Ingawa yeye katueleza ana pasipoti moja ya Tanzania na hiyo wanayosema si paspoti kama walivyosema, sasa tunasubiri tuone.”


Hadi jana usiku, Manji alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Tafa ya Muhimbili katika majengo ya Taasisi ya Moyo ya Jakata Kikwete.

No comments:

Post a Comment