Wednesday, August 29, 2018

KOCHA SIMBA AFUNGUKA SABABU YA KUMUWEKA BENCHI MO

Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amefunguka na kuweka hadharani sababu za kiungo wake, Mohammed Ibrahim kutokupata nafasi.

Tangu msimu wa ligi uanze, kiungo huyo hajapata nafasi ya kucheza kutokana na upana wa kikosi hicho ambao una wachezaji wa kila aina kulingana na usajili ambao imeufanya.

Mbeligiji amesema kikosi cha Simba ni kipana na kina wachezaji walio na ushindani, hivyo hawezi akamuanzisha kama waliopo kwenye kile cha kwanza wanafanya vizuri.

Aussems ameeleza kujituma kwa mchezaji ndiyo kutamfanya apate namba kwenye kikosi chake hivyo kama Ibrahim anataka namba inabidi apambane.

Kocha huyo tangu atue nchini kuanza kibarua na wekundu hao wa Msimbazi, hajapoteza mchezo hata mmoja uwe wa kirafiki au wa kimashindano mpaka sasa.

Tuesday, August 28, 2018

MFAHAMU BINT AMBAYE ANATABIRIWA KUWA NYOTA WA TEKNOLOJIA

Mwanafunzi Tomisin Ogunnubi ni kijana anayependa sana kutengeneza programu za kiteknolojia

Miaka mitatu iliyopita alitengeneza, programu ya My locator, inayowasaidia watoto waliopotea.

Programu hiyo ya simu ambayo inapatikana katika hifadhi ya Google tayari imeanza kupakuliwa zaidi ya mara 1000 tangu uzinduzi wake mwaka wa (elfu mbili na kumi na sita) 2016.

'Programu hiyo inaweza kukushirikisha na ramani ya Google na kukuonyesha maelezo ya mahali ulipo hadi katika eneo ulilohifadhi'', Tomisin ambaye sasa ana umri wa miaka 15 na anayesoma mjini Ikeja anaelezea.

Hatua za dharura
"Pia ina uwezo ambapo unapobofya kitufe cha dharura, inatuma ujumbe na kupiga simu -iwapo umeiwezesha hadi katika nambari uliopendelea".

"Inaweza kuwa nambari ya dharura ama nambari ya mtu wa familia. Ni chaguo lako. Hivyobasi iwapo kuna dharura, na unahitaji majibu ya haraka inatuma anwani yako kwa nambari hiyo ili mtu aweze kufahamu kwa haraka mahala ulipo''

"Nataka habari za haraka kuhusu usalama nikifikirie kwamba ….kuna watu hatari tofauti, hivyo basi nadhani wazo la kuweza kutoka nje na kuwa salama ndio lililonishinikiza kuanzisha programu hii", anaelezea.

"Lakini nilikuwa na umri wa miaka 12 nikifikiria kuhusu wazo hilo, na sasa nimejifunza jinsi ya kutengeneza programu. Kwa nini basi nisitumie nilichojifunza kutengeneza kitu ambacho kinaweza kuwa na manufaa kwangu mimi na watu wengine?''

Aniedi Udo-Obong meneja wa programu katika kampuni ya Google anasema kuwa kuna uhaba wa watu wa kuenziwa katika sekta hiyo nchini Nigeria huku watu wengi nchini humo wakienzi watu kama vile Elon Musk na mark Zuckerberg.

"Lakini wanafunzi zaidi wa vyuo vikuu wameanza kutambua sekta hiyo kama njia nzuri ya kujipatia kipato kupitia kuanzisha kampuni za kiteknolojia", anaongeza kusema.

Anedi mara kwa mara hukutana na wafanyibiashara wenye mawazo mengi katika kampuni ya Google. Kazi yake inashirikisha kuanzisha uhusiano na wavumbuzi ili kuimarisha mazingira Afrika. Anaelezea kwamba kuna haja ya kuimarisha programu ya my Locator , lakini anasema kuwa Tomisin tayari amepiga hatua muhimu.

"Ninafurahishwa na programu ya Tomisin kwa sababu mbili. Napendelea kuona bidhaa katika hali yoyote badala ya kusikia kuhusu wazo zuri zaidi. Napenda kusikia kwamba mtu amekuwa na wazo kichwani mwake na kuweza kulishughulikia na kukamilisha kitu'', anasema.

Vipaji vya vijana

Mwalimu wa Tomisin anayefunza somo la sayansi ya tarakilishi Kofoworola Cole anasema kuwa,ufanisi wa kijana huyo ulichangia pakubwa vile shule hiyo inavyofundisha somo hilo. Pia umechangia pakubwa katika kuwashinikiza wanafunzi katika shule hiyo.

''Ilitupatia motisha kuweza kuanza miongoni mwa watoto wenye umri wadogo, kawaida tuliwalenga wanafunzi wakubwa. Lakini wakati Tomisin alipofanikiwa tulijua kwamba ni kweli kuna vipaji katika madarasa yenye vijana wenye umri mdogo'', alisema

Aniedi anasema kuwa uwekezaji mkuu katika sekta ya elimu unahitajika ili kupunguza mwanya uliopo kati ya wanafunzi wanaotoka katika familia tajiri na wale wanaotoka katika jamii masikini.

"Tumeona mipango inayolenga madarasa ya watoto wadogo katika shule za msingi katika mataifa megine kama vile Estonia, Uingereza, China na Korea…nina hofu kwamba huenda tukawachwa nyuma iwapo hatutawahusisha watoto wetu katika kiwango kama hicho wakiwa na vifaa na teknolojia ambazo wenzao katika mataifa mengine na masoko wanatumia kujifunza'', anasema.

"Teknolojia ndio tegemeo la siku zijazo na kuweza kujua teknolojia ndio kuweza kutatua matatizo'', anasema Tomisin

'' Ninapenda teknolojia kwa sababu kuweza kuleta mabadiliko ni kitu ninachopenda kufanya''.

KUFIKIRIA KUACHA MUZIKI SIJUI, NAKUWA MZITO SANA KUSEMA ITAFIKIA SIKU NITASHINDWA KURAP-JOH MAKINI

Rapper Joh Makini kutoka kundi la Weusi, amefunguka kuhusu kufikiria kuacha muziki na kufanya ishu zingine.

Joh amesema hayo Jumatatu hii kwenye kituo cha radio cha EA Radio ambapo alipata fursa hiyo kwenye siku hiyo ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akiongeza kuwa haitokuja kutokea maishani mwake, kuacha kurap labda kifo ndio kiwe sababu ya yeye kumtenganisha na muziki.

“Kufanya vitu vingine tofauti katika maisha hilo ni muhimu kabisa, lakini kufikiria kuacha muziki sijui, kwa sababu nakuwa mzito sana kusema itafikia siku nitashindwa kurap?, Sijui ila napenda muziki sana”, amesema Joh Makini.
“Endapo ikitokea nikiacha kurap na kutoenda studio lazima nitakuwa kwenye mzunguko wa kufanya vitu vingine na muziki pia. Sioni sababu ya kuacha muziki labda kifo ndio kitanitenganisha lakini sio kitu kingine,"ameongeza.
Joh ameendelea kusema kuwa kwa sasa muziki wa Hip Hop nchini unalipa kwa kiasi kikubwa, tofauti na ulivyokuwa zamani huku akiwarushia dongo wasanii wanaolalamikia kuwa yawezekana wao wenyewe hawajajipanga katika kutoa kazi nzuri ndio maana wanayumba.

HAKIMU ALIYEHUKUMU KESI YA BILIONEA MSUYA ATISHIWA KUUAWA

Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya na kuwahukumu adhabu ya kifo washitakiwa watano, ametishiwa kuuawa na mtu asiyejulikana

Inadaiwa mtu huyo alipiga simu kupitia simu ya mezani(ofisini) na kumtisha kummiminia risasi kama za bilionea Msuya kwa kitendo cha kumhukumu ndugu yake kunyongwa

Mtu huyo alimwambia Jaji kuwa iwapo watashindwa kumuua nyumbani au barabarani, basi wangetekeleza mauaji hayo akiwa katika eneo la mahakama Kuu

Kutokana na vitisho hivyo, Jeshi la Polisi limemuongezea ulinzi Jaji huyo ambaye sasa amehamishiwa divisheni ya Ardhi jijini Dar lakini bado anamalizia kesi zake jijini humo

Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi na bunduki ya kivita aina ya SMG Agosti 7, 2013 eneo la Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

TRUMP NA KENYATTA WAJADILI UGAIDI NA BIASHARA

Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na mwezake wa Kenya Uhuru Kenyatta mjini Washington na kuzungumzia masuala mbalimbali, zaidi wakiangazia biashara na usalama.

Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya Marekani, wakati wa ziara hiyo mataifa hayo mawili yalikubaliana na kutangaza mikataba ya jumla ya $900 milioni.

Hata hivyo mazungumzo yao yaligubikwa na msiba wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Marekani na Seneta wa muda mrefu katika bunge la nchi hiyo John McCain.

Rais Kenyatta ni kiongozi wa tatu kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kukaribisha Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo na Rais Trump.

"Tumekuwa na ushirikiano mzuri na wa kipekee na Marekani katika masuala ya usalama na ulinzi, hasa katika harakati za kukabiliana na ugaidi. Muhimu zaidi tuko hapa kuboresha ufungamano wetu katika biashara na uekezaji, " kasema Rais Kenyatta.

Rais Trump alisema Kenya na Marekani zitaendelea kushirikiana kuimarisha ufungamano wao katika biashara, uekezaji na usalama.

"Tunafanya shughuli nyingi za utalii, biashara na ulinzi. Na kwa wakati huu tunajibidiisha kuboresha usalama," alisema Rais Trump. " Tunafurahia sana kuwa nawe hapa."

Viongozi hao wawili walijadiliana pia kuhusu safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York zitakazoanza mwezi Oktoba mwaka huu na kukubaliana kwamba safari hizo za ndege zitaimarisha zaidi utalii na biashara kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Marekani ndiyo chanzo kikuu cha watalii wanaozuru Kenya na taifa hilo la Afrika Mashariki linatarajia kutumia fursa ya safari za moja kwa moja za ndege za Kenya Airways kati ya mataifa hayo mawili ambazo zitaanza Oktoba 28 kuimarisha idadi ya watalii wanaofika kenya.

Viongozi hao wawili kwa pamoja wamejadili njia za pamoja za kupambana na ugaidi na ushirikiano wa kibiashara.

Mpango wa upanuzi wa barabara inayohusisha miji mikubwa ya Kenya, Mombasa na Nairobi pia ilijadiliwa.

Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba amefanikisha makubaliano yenye thamani ya mamilioni ya dola na Wawekezaji wa Kimarekani.

Katika siku za hivi karibuni China imeipita Marekani kwa kuwa na uwekezaji mkubwa nchini Kenya.

Hata hivyo Rais Kenyatta ameonekana kuwa na bidii ya kuwakubali washirika wote kibiashara.

Kibiashara, Kenya ni ya 85 kwa kuiuzia Marekani bidhaa duniani na wa jumla biashara kati ya mataifa hayo mawili huwa ya thamani ya jumla ya dola 1.5 bilioni za Marekani kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya Marekani.

Kenya imekuwa ikitafuta ufadhili wa ujenzi wa barabara mpya kuu ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, mradi unaotarajiwa kugharimu takriban dola 4.5 bilioni za Marekani.

Kenya hutazamwa kama mshirika muhimu wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi Afrika Mashariki na katika Upembe wa Afrika.

Mataifa yote mawili yana majeshi Somalia yakikabiliana na wapiganaji wa al-Shabaab.

Baadaye wiki hii pia anatarajia kumpokea jijini Nairobi, Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, kabla ya kufunga safari kuelekea Beijing, kwenye mkutano wa pamoja wa Afrika na China.

Monday, August 27, 2018

HII NDIO HATMA YA ALIKIBA COASTAL UNION

KOCHA wa Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa nyota wake mpya, Ally Salehe Kiba ‘Ali Kiba’ ana nafasi kubwa ya kucheza mechi zijazo licha ya kuwa na majukumu mengine ya kimuziki chini Canada kwa sasa.

Hadi sasa licha ya Coastal Union kucheza michezo yake miwili ya Ligi Kuu Bara, Kiba hajaonekana uwanjani kutokana na kubanwa na shughuli zake za kimuziki. Alikwenda Canada tangu wiki moja iliyopita na inaelezwa kuwa jana Jumapili alitoka huko kuelekea Afrika Kusini kumsalimia rafiki yake Ommy Dimpoz ambaye amelazwa kutokana na tatizo la koo, na hali yake ni tete.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgunda amesema amefanya mazungumzo ya kina na Kiba na ana nafasi kubwa ya kuwepo kwenye kikosi kitakachotumika katika mchezo ujao dhidi ya KMC Jumamosi hii, na kudai kuwa hana wasiwasi na uwezo wake kwa kuwa anafahamu ni mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu.

“Labda nikuambie tu sisi tumesajili wachezaji zaidi ya 30 akiwemo Ali Kiba, hivyo wote wana nafasi ya kucheza kwenye timu yetu.

“Na kuhusu Kiba, hapana shaka kuwa atacheza mechi zijazo kwa sababu nishafanya naye mazungumzo na ninajua ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa,” alisema Mgunda.