Monday, July 30, 2018

WAZIMBABWE KUFANYA UCHAGUZI WA KWANZA TANGU MUGABE AONDOLEWE

Wapiga kura Zimbabwe wanaelekea debeni katika uchaguzi wa kwanza pasi kuwepo kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe miongoni mwa wagombea.

Kiongozi huyo muanzilishi, Mugabe alitimuliwa katika mapinduzi mwaka jana baada ya kuwa madarakani kwa takriban miongo minne.

Wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais ni kiongozi aliyepo Emmerson Mnangagwa,wa chama tawala Zanu-PF na kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa.

Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa pia zinafanyika leo Jumatatu.

Kura za kutafuta maoni zinampa uongozi mdogo Mnangagwa, mwenye miaka 75, dhidi ya mpinzani wake mwenye miaka 40 anayekiongoza chama cha Movement for Democratic Change (MDC).

Hapo jana kiongozi wa zamani Robert Mugabe - aliyeingia kwa mara ya kwanza madarakani mnamo 1980.

Kunashuhudiwa idadi kubwa ya watu wanaopiga kura kwa mara ya kwanza nchini , ambako kura ya vijana ndio inayotazamwa kuwa na uzito. Takriban nusu ya watu waliosajiliwa kupiga kura wapo chini ya miaka 35.

Mamia ya waangalizi wametumwa kuhakikisha uchaguzi unakwenda sambamba, lakini mara kwa mara upinzani umetuhumu kuwepo udanganyifu katika daftari la wapiga kura.

Wameelezea wasiwasi pia kuhusu usalama wa makaratasi ya kupiga kura na kunyanyaswa kwa wapiga kura hususan katika maeneo ya mashinani.

Uchaguzi huo unafuata miongo kadhaa ya utawala wa unyanyasaji uliosababisha changamoto kubwa za kiuchumi kwa taifa hilo.

Hili linajumuisha masuala ya uwekezaji, elimu, afya na ajira - takwimu kadhaa zinaashiria kwamba ukosefu wa ajira upo juu kwa 90%.

Rais Mnangagwa, anayejulikana kama "Mamba" ameahidi kuhakikisha kuna nafasi za ajira na anaonekana kukubali kuidhinisha mageuzi ya kiuchumi.

Ameponea majaribio kadhaa ya kuuawa ambapo wafuasi wa Mugabe wanatuhumiwa kuyatekeleza.

No comments:

Post a Comment