Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura na kusema sababu kubwa ya kusogezwa mbele mchezo huo ni kutokana na wamiliki wa uwanja huo kuwa na shughuli ya kijamii kwenye uwanja siku ya April 20.
Simba itarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumamosi huku ikiwa na alama 58 pekee ambapo inaifanya timu hiyo mpaka sasa kuendelea kushika usukani wa ligi, nafasi ya pili ikichukuliwa na watani wao jadi Yanga kwa alama 47, Azam FC akishika nafasi ya tatu kwa alama 46.

No comments:
Post a Comment