Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Obrey Chirwa kutocheza dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia kutokana na adhabu yakadi za njano alizopata dhidi ya Township Rollers ya Botswana, Mzimbabwe, Donald Ngoma anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Mzambia huyo.
Ngoma alianza mazoezi katika kikosi cha Yanga hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kulikosababishwa na majeraha.
Yanga itacheza na Wolayta Dicha Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo wapinzani wao hao wanatarajia kuwasili jijini kesho.
Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema kuwa, tayari kikosi chao kimeshaanza mazoezi kwa ajili ya kuwakabili Waethiopia hao huku mshambuliaji wao Donald Ngoma akionyesha matumaini makubwa ya kucheza mchezo huo.
“Tayari tumeshaanza maandalizi kwa ajili ya wapinzani wetu Wolayta Dicha kwa kuanza mazoezi leo ‘jana’ kuelekea mchezo huo ambao tunahitaji kushinda.
“Mshambuliaji wetu Ngoma yupo fiti tangu alipoanza mazoezi na kuna uwezekano mkubwa wa kucheza iwapo mwalimu ataamua kumpanga kwa kuwa hana tatizo lolote na anaonyesha matumaini makubwa,” alisema Hafidhi.
No comments:
Post a Comment