Friday, February 16, 2018

WAZIRI MKUU AAGIZA WAKANDARASI KUKAMATWA,KUSHTAKIWA

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ameagiza wakandarasi watatu wanaotekeleza miradi ya maji halmashauri ya Buchosa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutekeleza miradi hiyo wenye gharama ya Sh1.3 biloni chini ya kiwango.

Pia, ameagiza halmshauri hiyo kukikisha zinawasainisha mikataba wakandarasi wenye uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali inayotengwa kwenye halamshauri hizo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo jana Februari 15, 2018 katika halmshauri ya Buchosa baada ya kuzindua jengo la hospitali ya halmashauri hiyo lenye thamani ya Sh540 milioni.

Baada ya kuzindua jengo hilo alisema jambo linalotesa wananchi katika halmashauri hiyo ni maji amabayo miradi yake inasuasua.

Sakata hilo lilianza baada ya Majaliwa kumtaka mhandisi wa maji wilaya ya Sengerema, Magembe Makara kueleza hali ya mradi wa maji wa Umeya, Kalebezo hadi Nyehunge ulioanza kutekelzwa mwaka 2012.

Wananchi walianza kuzomea baada ya mwandisi huyo kudai kuwa mradi huo upo kwenye uangalizi na maji yanatoka.

Hali hiyo ilimfanya Waziri Mkuu kumtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Anthony Sanga kuthibitisha iwapo kauli ya Mhandisi huyo ni sahihi, ambapo Sanga alisema mradi huo unakabiliwa na changamoto kadhaa.

Mbunge wa Buchosa, Charles Tizeba ndiye aliwawashia moto watendaji hao baada ya kumweleza Waziri Mkuu kuwa utekelezaji wa mradi huo unakwamishwa na ushauri mbovu wa mkandarasi mshauri.

"Kuna matatizo mengi katika mradi huu ikiwemo mabomba kupasuka; kiukweli ni kama hakuna mradi wa maji uliokamilika kwa sababu ubovu uliopo unalazimisha uanze upya,” alisema Tizeba ambaye pia ni waziri wa Kilimo.

Tizeba alimwagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale kutoa ufafanuzi taasisi hiyo imechukua hatua gani kuchunguza suala hilo.

Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Makale alisema jalada la suala hilo limefikishwa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa uamuzi  baada ya uchunguzi wake kukamilika.

Kutokana na hali hiyo Majaliwa alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kufuatilia suala hilo likiwemo jalada lililoko ofisi ya DPP kushughulikiwa haraka ili watuhumiwa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment