Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia Bin ameeleza kuwa kikosi hicho kitafanya mazoezi kwenye Uwanja huo kwa siku tatu kabla ya kuhamia Uwanja wa Uhuru.
Tayari Msuva, mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga yupo nchini, wakati Samatta mchezaji wa zamani wa Simba SC anatarajiwa kuwasili usiku wa leo.
Kwa ujumla kikosi kiliochoteuliwa na kocha Salum Shaaban Mayanga kwa ajili ya mchezo huo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).
Mabeki Gardiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (BarokaFC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).
Viungo ni Himid Mao ambaye pia ni Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Yanga) na Mbaraka Yussuph (Azam FC).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
No comments:
Post a Comment