Wolper akiwa na Mpenzi wake Brown
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu Wolper amesema watu wanadai mpenzi wake ni mbeba pochi lakini anachojua ni wivu ndiyo unaowasumbua kwa sababu wanafahamu kazi anayofanya lakini kwa kuwa yeye anathamini kazi ya mpenzi wake huyo lazima atahakikisha anamvusha boda kwa kutumia mtandao alionao.
"Kuna mtu anamuita 'BFF' mbeba pochi, najua anafahamu ni kazi gani anafanya lakini kwa kuwa anaumia lazima amchafue. Mpenzi wangu ni 'model' ambaye ameshafanya kazi nyingi tu za kutembea majukwaani lakini si unajua sekta za mitindo hapa nyumbani?, hazijazingatiwa sana kwa hiyo mimi kwa kuwa tayari nina 'connection' nje nitampigania kuona anafanya kimataifa zaidi na siyo nyumbani" Wolper
Akizungumzia kuhusu mpenzi wake huyo kutumika kama mpendezeshaji video 'Video King' "Suala la kutumika kama 'video King' hapa nchini sitaki kabisa kusikia wala kuona kwa sababu hakuna maslahi, na mpaka sasa jiandaeni kuona 'suprise' kwani tayari kuna 'dea'l za kazi za South Afrika tumeshasaini mikataba kwa hiyo mambo ni mazuri upande wetu".
Mbali na hayo Wolper amesema haogopi kumsaidia mpenzi wake kwa hofu ya kuja kusalitiwa mbeleni kwani anaamini Mungu amempatia Brown kwa kuwa ana vigezo vyote anavyohitaji na hata ikitokea akamsaliti hatakuwa na shida kwani atakuwa daraja la mafanikio yake.
No comments:
Post a Comment