Monday, September 18, 2017

MANARA AMWAGIA SIFA OKWI

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amefunguka na kudai hakuna kama mchezaji Emmanuel Okwi Afrika Mashariki nzima kwa sasa, japo timu ya Yanga iliwacheka kipindi wanamsajili na kumuita jina la muhenga.


Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba kuanza vizuri katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuifungia mabao sita mpaka sasa timu yake,katika mechi mbili na kuweza kuzima maneno ya wapinzani wao waliyokuwa wanamuita muhenga kipindi alipokuwa akisajiliwa kwa madai kiwango chake kimeshakwisha katika kulisakata kabumbu.

"East Afrika ina Okwi mmoja tu, 'game' mbili goli sita mara mbili ya magoli yote ya Gongowazi kwa michezo yao mitatu. Kosa lao lilikuwa kumwita mhenga, atashinda kila tuzo nchi hii, 'this is Simba and that is Okwinho", ameandika Manara.

Kwa upande mwingine, klabu ya Simba inatarajiwa kushuka katika dimba la CCM Kirumba Mkoani Mwanza Septemba 21 mwaka huu dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment