Thursday, August 3, 2017

YAMETIMIA SASA MESSI AMUAGA RASMI NEYMAR


 Baada ya tetesi na maneno mengi hatimaye muda umefika na tetesi zote zimekuwa kweli, Neymar hatavaa tena uzi wa Barcelona na jina lake halitakuwepo kwenye MSN.

Neymar anaondoka, Lioneil Messi amethibitisha hilo na kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter amemtakia kila la kheri swahiba wake huyo katika maisha yake mapya Ufaransa.

“Nimefurahi kuwa na wewe na kucheza na wewe rafiki yangu na nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya ya soka unayoenda kuanza” aliandika Messi kupitia Instagram.

Kauli ya Messi inakuja ikiwa ni masaa machache tangu Neymar aondoke katika uwanja wa mazoezi na klabu hiyo imetoa taarifa kwamba Neymar amepewa ruhusa kwenda kumalizana na PSG.

Usajili wa Neymar kwenda PSG utavunja rekodi zote zilizowahi kuwekwa duniani kwani PSG watatoa kiasi cha £200m ikiwa ni mara mbili na zaidi ya kiasi cha rekodi ya uhamisho wa sasa wa dunia inayoshikiliwa na Paul Pogba.

No comments:

Post a Comment