Wednesday, August 2, 2017

HALMASHAURI YA KISARAWE WAPATA HATI SAFI

Halmashauriya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka 2016 imefanikiwa kupata hati safi baada ya wakaguzi wenye dhamana ya kazi hiyo kutekeleza majukumu ya kazi zao.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Hamisi Dikupatile katika kikao maalumu kilichojadili hoja za Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka huo wa fedha ambapo alisema wana-Kisarawe sana kila sababu ya kufurahia hatua hiyo inayotokana na kazi nzuri za Watendaji, Madiwani, Wananchi, Mkaguzi wa ndani ambaye ndo jicho lao pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.

Kikao hicho ambacho ofisi ha Mkuu wa Mkoa iliwakishwa na Rashid Baghdellah kutoka ofisi ya Serikali za Mitaa, pia kilihudhuliwa na Mkaguzi Mkazi mkoa Eliuther Masombola aliyeambatana na wataalamu wake, Mkuu wa wilaya Hapiness Seneda, Mbunge Viti Maalumu Mkoa Zaynabu Vullu na Kaimu Mkurugenzi Wanchoka Chichibela ambapo Dikupatile alisema hiyo inatokana na kazi nzuri iliyofanywa na watumishi wa kada zote.

"Tunawapongeza wote waliofanikisha upatikanaji wa hati safi, tunajipanga kuhakikisha tunaanza utaratibu wa kumwezesha Mkaguzi wetu wa ndani ili aweze kufika maeneo yote katika kufanyakazi yake vizuri, kwakweli anafanyakazi kwa ufanisi mkubwa na leo hii tunathibitisha ubora huo, pia tunawapongeza wana- Kisarawe kwa umoja wetu, madiwani na watumishi wote," alisema Dikupatile.

Akizungumza katika baraza hilo, Masombola alisema kuwa ofisi yake imefarijika kuona kazi nzuri iliyofanywa na halmashauri na hatimae kuweza kupata hati safi, huku akiwaomba juhudi hizo ziendelezwe ili kuhakikisha kila mwaka wanapata hati hiyo, na hiyo naonesha ni namna gani wahusika wa masuala ya fedha wanavyotekeleza majukumu yao kwa kuzingatia, sheria, haki na taratibu zinazowaongoza katika kutekeleza kazi zao.

"Hii ni uthibitisho tosha kwamba wana-Kisarawe kila mmoja katika nafasi yake anatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, haki na wajibu, haya ni matunda ya kazi yenu ambayo imeongozwa na Mkaguzi wenu wa ndani kwa kipindi kilichoushia mwaka wa fedha Juni 30. 2016, ongereni sana," alisema Masomola.

Kwa upande wake Baghdellah aliwapongeza watendaji kwa kusimamia vizuri sheria za fedha na kuhakikisha wanafanya vizuri na hatimae kupata hati safi, aidha aliongeza kwamba katika taarifa iliyowasilisha za Mkaguzi ameona kuna hoja aina mbili, ya kwanza kama wametoa hoja kwenye taasisi ambazo zilitakiwa kutekeleza majukumu yao lakini hawakufanya, ya pili ikiwataka watendaji wa halmashauri watekeleze wajibu wao.

"Kuhusu upungufu wa watumishi halmashauri haiajili, vibali vinatoka huko, hoja nyingine ni suala la hela mlizosaidia Wizara ya ardhi, tunawaomba Wakaguzi wasituhoji, ushauri unaotoka kule watusaidie, tuchukulie utaratibibu wa utumishi mfano una upungufu wa watumishi 300 unapeleka ombi mnajadiliana mpaka mnafikia mwafaka, mkiafikiana inapofika mwezi wa 7 waajiliwe sio kucheleweshwa vibali," alisema Baghdellah.

No comments:

Post a Comment