Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee amesema kuwa anasikitishwa na jeshi la polisi kushindwa kuwakamata matapeli ambao wamekuwa wakitapeli wananchi kwenye mitandao kupitia jina lake.
Amesema kuwa ni muda mrefu alishatoa taarifa jeshi la polisi kuhusu watu hao wanaotumia jina lake kwenye mitandao ya kijamii na kujifanya kutoa mikopo yenye riba ndogo na kuwatapeli wananchi pesa zao.
“Wanaojitambulisha kutoa mkopo kwa jina langu ni matapeli, sihusiki na chochote na hao matapeli na nmeshatoa taarifa polisi inaonekana hawakamatiki” amesema Halima Mdee
No comments:
Post a Comment