Kamanda Magiligimba
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba, amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27 katika kijiji cha Kijota wakati lori hilo likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini ambapo amebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva.
Kamanda Magiligimba amesema dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka hakuwa makini na barabara wakati anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi.
Aidha waliofariki wametajwa katika ajali hiyo ni pamoja na Haji Jumanne, Mikidadi Mohammed wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama, Musa Salimu mkazi wa kijiji cha Mwakiti, wengine ni Allen Mwangu mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari mkazi wa kijiji cha Ilongero.
Akizungumzia majeruhi wa ajali hiyo Kamanda Magiligimba amesema kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, 10wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.
No comments:
Post a Comment