Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ambaye hivi karibuni amejiunga na Simba.
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ahmed Iddi Mgoyi ametangaza kutogombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao wa shirikisho hilo. Kupitia waraka wake uliotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, Mgoyi ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji kwa muda mrefu kuliko wote akishika nafasi hiyo kwa miaka 13, amesema anadhani huu ni wakati wa wengine nao kuonyesha uwezo wao wa kiuongozi.
“Nawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF katika chaguzi tatu za TFF kwa kuonyesha imani na mimi. “Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake chini ya Rais Jamal Malinzi kwa ushirikiano uliotukuka na nitawakumbuka sana kwa mengi mchanganyiko.
Beki wa zamani wa Simba, Ashanti United, Coastal Union na Mbeya City, Juma Nyosso.
Mpaka anatangaza kutogombea, Mgoyi ni mjumbe Kamati ya Utendaji ya TFF akiwakilisha mikoa ya Kigoma na Tabora tangu mwaka 2004.
VIONGOZI wa timu ya Yanga wameamua kufanya kweli baada ya kumalizana na beki ‘kisiki’ wa Mbao FC ya Mwanza, Asante Kwasi, raia wa Ghana na inadaiwa amepewa mkataba wa miaka mitatu. Mghana huyo alikuwa mgumu kupitika na aliwazuia vyema washambuliaji wa Yanga pale walipokutana na anakumbukwa kwa urahisi kutokana na kuisaidia timu hiyo kushinda mara mbili walipokutana.
Championi Ijumaa limetaarifiwa kuwa, tayari beki huyo amefanikiwa kumalizana na Yanga, hivyo muda wowote atatangazwa rasmi kuitumikia timu hiyo. “Usajili wa mwaka huu ni wa aina yake, maana utaona kuna watu ambao hata hatujategemea wanasajiliwa, kama huyu Asante Kwasi, habari za wazi tayari Yanga wamefanikiwa kumalizana na beki huyo Mghana na muda wowote ataitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu,” kilisema chanzo hicho. Katibu wa Mbao FC, Richard Athanas, ameliambia
Championi Ijumaa: “Hata mimi nimesikia taarifa hizo za Yanga kumsajili Asante Kwasi japo ninavyojua bado ana mkataba na sisi, na nimeshindwa kumuulizia kwa sababu jana usiku (Jumanne hii), wakati napata taarifa hizi, sikuweza kumpata hewani, maana tayari alikuwa ameshapanda ndege kuelekea kwao Ghana, hivyo ukweli na uhakika nitaupata nitakapofanikiwa kuongea naye,” alisema Athanas.
Hata hivyo, imebainika kuwa kabla ya Nyosso kutua Kagera Sugar, uongozi wa Simba ulikuwa na mpango wa kutaka kumsajili ili kuziba pengo la Mzimbabwe, Method Mwanjale ambaye anaweza kufungashiwa virago muda wowote kutokana na umri wake kuwa mkubwa. Hata hivyo, kitendo cha uongozi huo wa Simba kumsajili Bocco kilibadili upepo na ndipo ulipoamua kumpotezea beki hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mmoja wa viongozi wa Simba alithibitisha hilo na kusema sababu kubwa ni kukwepa mpasuko ndani ya timu hata kama walikuwa wameshayamaliza wao wenyewe. Nyosso alipoulizwa juu ya suala hilo alisema: “Hawakuwa na nia ya kunisajili mbona mimi na Bocco tupo vizuri na hatuna tatizo lolote, nilimuomba msamaha na yeye akanisamehe kwa hiyo kama ni kufanya kazi tungefanya tu bila ya tatizo lolote lile.” Wachezaji wengine waliojiunga na Kagera juzi ni Hussein Kipao (JKT Ruvu), Japhary Kibaya (Mtibwa Sugar), Peter Samson Mwalyanzi, Ludovick Venance na Omary Daga (African Lyon).
No comments:
Post a Comment