Wednesday, May 24, 2017

VYOMBO VYA UTANGAZAJI VYASHTAKIWA KWA SERIKALI


Dar es Salaam. Viziwi wameitaka Serikali kuvisimamia vyombo vya utangazaji kuweka wakalimani wa lugha za alama ili waweze kufahamu mambo yanayoendelea nchini.
Akizungumza leo, Jumatano Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita),Nidros Mlawa amesema viziwi ni walipakodi kama ilivyo kwa wananchi wengine hivyo wana haki ya kupata taarifa.
"Tunabaguliwa wakati sisi pia ni walipakodi, televisheni hata ya Taifa haina wakalimani wa lugha hatujui nchi inaenda vipi,"amesema.
Amesema wakati umefika kwa wamiliki wa vituo vya utangazaji kuanza kutoa huduma hiyo kama ambavyo kanuni za utangazaji zinavyotaka waweke wakalimali.

No comments:

Post a Comment