Thursday, May 25, 2017

EPUKA MAMBO HAYA KAMA UNATAKA MAFANIKIO YA KWELI KATIKA MAISHA YAKO


"Hivyo ulivyo inatokana na mtazamo ulionao" usemi huu niliwahi kukutana nao siku moja katika pekuapekua zangu, usemi huu una ukweli ndani yake kwa asilimia zote uzijuazo wewe, kwa sababu maisha yako hivyo yalivyo yanataokana na mtazamo na imani ulizonazo.
Watu wengi ambao hawajafanikiwa wanaamini ya kwamba mafanikio yanapatina kwa baadhi ya watu fulani, lakini dhana hii si kweli kwa sababu kila mmoja mwenye pumzi na fikra ana wajibu wakuweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio makubwa yatakuwa upande wako endapo utaacha mara moja kulalamka juu ya mambo yautayo;
1. Acha kulalamika juu ya elimu uliyonayo.
Mafanikio yatakuja kwako endapo utaacha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Watu wengi wanalalamika eti kwa sababu ya elimu walizonazo, wengi husema mimi sina mafanikio kwa sababu sina elimu ya kotosha, au nimesoma kidogo na sina elimu ya chuo kikuu.
Kiuhalisia, dhana hii haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio yako, hii ni kwa sababu sio kila mwenye elimu amefanikiwa hivyo kwa elimu hiyohiyo ambayo unayo ni kigezo tosha juu ya mafanikio yako. Hebu tujiulize watu wengi ambao wamefanikiwa elimu zao ni kiwango gani?
2. Acha kulalamika eti hujafanikiwa kwa sababu huna bahati.
Kama nilivyoanza kueleza hapo awali ya kwamba mtazamo ndio kila kitu, imani hii ya kuendelea kuamini ya kwamba mafanikio ni bahati nakuomba uachane nayo mara moja, imani hiyo inaweza kukupoteza na ukashindwa kupata mafanikio kama utaishikilia sana.
Tambua imani kubwa juu ya mafanikio ni kwamba kila mmoja amezaliwa kwa ajili ya kufanikiwa na si vinginevyo jambo la msingi ni kwamba mara zote hakikisha unakuwa na mtazamo chanya, ubunifu, pamoja kufanya kazi kwa bidii haijalishi ni kazi ndogo au kubwa kiasi gani.
3. Acha kulalamika eti huna pesa za kutosha.
Hili ndilo kikwazo cha mafanikio ya wengi hii ni kwasababu watu wengi wamekuwa wanalalamika ya kwamba hawana pesa za kutosha ili wafanye jambo fulani, kuendelea na tabia hii ni kujiua mwenyewe kwani siku zote pesa huwa hazitoshi.

Jambo la msingi ni kuhakikisha kwa kiwango hicho cha pesa ulichonacho ni njia pekee ya kuanza kufanya jambo unalolitaka, kwani endapo utaendelea kusubiri ufikishe kiwango fulani cha pesa ndio uanze kufanya jambo fulani nakuhakikishia huwezi kufanya kamwe.
4. Acha kulalamika juu ya serikali kama kweli unataka kufanikiwa.
Maisha yako yapo mikononi mwako, hata hivyo kama kweli unaamini hili hakikisha unakuwa bora sana katika kutafuta kusudio lako katika dunia hii, nasema hivi kwa sababu watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wao kazi yao ni kuilaumu serikali tu.
Na watu hao wamekuwa wakifanya hivi huku siku sikizidi kwenda na wao maisha yao yamekuwa hayabadiliki,  jambo la msingi ambalo nataka kukuasa ni kwamba kila mmoja asimame kidete katika kuyapigania maisha yake ambayo yatamtengezea kesho yake bora.
Hivyo nikuache kwa kukuambia ya kwamba endapo utaendelea na tabia yako ya kulalamika ni kutengeneza maisha yako kuwa duni zaidi.
Nukuu ya siku inasema "kulalamika ni adui namba moja wa mafanikio yako"

No comments:

Post a Comment