Jana
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura kuchagua wabunge
watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.
Baada
ya mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa
Bunge, Job Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa
kuiwakilisha nchi.
Tanzania
inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana
yalitangaza washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura
nyingi za hapana, na hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.
Kati ya wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama cha Wananchi (CUF).
Wagombea wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za hapana.
- Fancy Nkuhi (CCM)
- Happiness Legiko (CCM)
- Maryam Ussi Yahya (CCM)
- Dkt Abdullah Makame (CCM)
- Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)
- Alhaj Adam Kimbisa (CCM)
- Habib Mnyaa (CUF)
Baada
ya matokeo hayo kutangazwa, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa
habari nje ya ukumbi wa Bunge alisema kuwa, hawayakubali matokeo hayo na
kuwa watakwenda mahakamani.
Mbowe
pia amemtuhumu Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kuhusika katika mchakato wa kuwakataa wagombea wa CHADEMA na kusema
kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka
kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa na kasoro.
No comments:
Post a Comment