Wednesday, April 12, 2017

MANARA AWAJIBU YANGA

Baada ya kamati tendaji ya Yanga kupitia kwa mjumbe wake Salum Mkemi kutanganza kupinga malalamiko ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa kumtumia mchezaji wao Mohamed Fakih kwenye mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba, afisa habari wa Simba Haji Manara ametoa taarifa rasmi akiwataka Yanga kutulia.

Kuna taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.

Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano.

Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari,pia waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale,,ni kushangazwa kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu,Hii ni rufani ya Simba dhidi ya Kagera sio wao Yanga.

Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha

Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.
IMETOLEWA NA.. Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA

No comments:

Post a Comment