Wednesday, April 12, 2017

KAMPUNI YA WANAMITINDO YA DONALD TRUMP KUFUNGWA

Shirika la wanamitindo la Donald Trump lafungwa baada ya miaka 18
kampuni ya wanamitindo liliyoanzishwa na rais Donald Trump mwaka wa 1999 litafunga milango yake kwa mara ya mwisho, ripoti zimeashiria.

Katika barua pepe inayosemekana kusomwa na shirika la habari la New York Post na Mother Jones, msimamizi wa wanamitindo wa Trump Corinne Nicolas anasemekana kugundua kuhusu kufungwa kwa shirika hilo

Mnamo wiki jana, wafanyakazi walisema kuwa shirika hilo lilikuwa linafanya kazi kwa kawaida, lakini katika ile barua pepe, ilisema kuwa linataka kuangazia biashara nyingine.

Donald Trump anamiliki asilimia 85 ya kampuni, ambayo awali ilijulikana kama TModels.

Kampuni hiyo imewakilishwa na wanamitindo maarufu akiwemo Mia Kang, Paris Hilton na mwanamtindo wa Uingereza Jodie Kidd.

Hata hivyo, barua pepe hiyo inayosemekana kuonekana na Mother Jones, Corinne Nicolas anasema kuwa shirika hilo la Trump linajiondoa kutoka kwa sekta ya wanamitindo.

"Tunajivunia nafasi ambazo tumepatia watu wengi wenye talanta"

Tangazo hilo limezuka baada ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa kitambo kwamba Trump aliwalazimisha kuishi katika mazingira duni.

Wanamitindo wawili kutoka kwa shirika hilo waliiambia Business Insider kwamba uzoefu wa wanamitindo wa Trump na wale wa mashirika mengine hauna tofauti.

Wanasema kuwa kampuni hiyo iliwatoza kodi ghali za nyumba ambazo zilikuwa na nafasi ndogo ya kuishi huku wakidaiwa fedha zaidi za ada na matumizi.

Madai hayo pia yalisema kuwa shirika hilo lilikuwa na historia ya kuwaandika kazi wanamitindo kutoka nchi za kigeni bila kuwa na vibali vya kufanya kazi.
Donald Trump na Ximena Navarrete, Mshindi wa pili wa shindano la Miss Universe 2010

Tangu kuchaguliwa kwa Donald Trump, wanamitindo na wafanyakazi wamekuwa wakiondoka kutoka kwa shirika lake.

Wataalamu katika sekta hiyo wanasema kuwa hili limetokana na utata unaomzunguka Trump katika ulingo wa siasa ambao umelifanya shirika lake kuwa na jina baya katika sekta ya wanamitindo.

No comments:

Post a Comment