Baada ya Kagera Sugar kuibana Simba siku ya Jumapili na kuichapa 2-1
kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Jumapili ya juma lililopita kwenye
uwanja wa Kaitaba, Dauda alifanya mahojiano kwa njia ya simu na golikipa
mzoefu nchini Juma Kaseja ambaye alikua kikwazo kikubwa kwa Simba siku
ya mechi hiyo.
Kaseja alikua bora kwenye mechi ile ndipo Dauda akataka kujua uimara huo wa golikipa wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ unatokana na nini hasa katika kipindi hiki ambacho watu wengi wanambeza kwa kumuita mzee.
“Mpira ni mchezo ambao unahitaji ushindani, mpira unahitaji wachezaji wawe fiti kwahiyo kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba tuliamua kujitolea kadiri tuwezavyo ili tuweze kupata pointi tatu,” alisema Kaseja ambaye ataendelea kukumbukwa ndani ya Msimbazi kwa kuwa miongoni mwa wachezaji walioitoa Zamalek ya Misri (mabingwa watete) kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika mwaka 2003.
Kaseja alipoulizwa nini kinachomfanya kuwa bora hadi kushinda tuzo ya mchezi bora wa mwezi alisema, mazoezi, kujitoa, kusikiliza malekezo ya walimu na ushirikiano na wachezaji wengine ndiko kunamfanya aendelee kutamba.
“Kikubwa ni jitihada za mazoezi, mpira ni lazima ujitolee tofauti na kipaji ulichonacho unatakiwa kusikiliza na kufuata maelekezo ya walimu kujituma mazoezini, kushirikiana na wenzako pamoja na benchi la ufundi kumefanya performance irudi kwenye hali yake.”
Mbali na mambo ambayo ameyataja Kaseja ambayo ndiyo hasa yanayomfanya awe bora, Dauda alihitaji kujua kitu pekee kinachowafanya Kagera Sugar kufanya vizuri msimu huu na kuwa kwenye nafasi tatu za juu zikiwa zimebaki mechi tano ligi kufika mwisho.
“Mimi nimejiunga na timu raundi ya pili ya msimu huu nimekuta timu imejiwekea malengo yake, baada ya mimi kujiunga na Kagera Sugar nilizungumza na mwalimu akaniambia malengo ya timu ikiwa ni pamoja na kumaliza katika nafasi za juu.”
“Alikuwa ananiomba nije nicheze Kagera lakini pia nimsaidie ku-organize wachezaji uwanjani na nje ya uwanja kwa hiyo kwa sababu tayari mwalimu alikuwa na malengo timu imalize katika nafasi za juu, nil;ipokuja Kagera nikakuta wachezaji pia wapo katika malengo hayo ya mwalimu kwamba timu imalize katika maliza nafasi za juu.”
“Kwa hiyo nadhani kila mchezaji anafanya majukumu yake uwanjani na nje ya uwanja tuweze kufikia hapo tulipofika, lakini kikubwa nachoweza kusema ni kwamba, bado kuna mechi tano malengo bado yako palepale tuweze kumaliza katika nafasi za juu na ikiwezekana tugombee nafasi ya kuchukua ubingwa kwa sababu nafasi hiyo bado ipo wazi.”
Kagera Sugar ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 25 pointi moja mbele ya Azam FC, inazidiwa pointi 11 na Yanga ambao ndio vinara wa ligi hadi sasa huku wakiwa pointi 10 nyuma ya Simba ambao wapo nafasi ya pili.

No comments:
Post a Comment