Wednesday, April 12, 2017

Baloteli apita Mlangoni kwa Kuserereka

KAMA unafikiria kuwa kuna siku Mario Balotelli ataacha vibweka, basi futa hilo akilini mwako. Hivi karibuni aliwaacha hoi maofisa usalama wa Uwanja wa Ndege nchini Ufaransa, baada ya kuingia mlangoni kwa ‘style’ ya kuserereka kwa magoti.

Tukio hilo lilitokea baada ya kuiongoza timu yake ya Nice kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lille.

Nice walikuwa wameshapachikwa bao moja na Lille, lakini mtukutu huyo alisawazisha kabla ya kuongeza jingine.

Wakati kikosi hicho kikiwa uwanja wa ndege baada ya safari hiyo ya kuwafuata Lille, Balotteli alitumia magoti yake kuserereka na kupita katika mlango waliokuwa wamesimama walinzi.

Kituko hicho hakikuwavunja mbavu wachezaji wenzake pekee, bali hata walinzi hao ambao walithibitisha ‘wendawazimu’ wa Muitalia huyo.

No comments:

Post a Comment